Thursday, October 13, 2011

BLACKBERRY NETWORK FAILURE

Watumiaji wa simu za mkononi aina ya BLACKBERRY duniani jana jumatano inasemeka wamekuwa wakipata matatizo kuunganishwa au kuconnect kwenye mtandao ikiwa sababu kubwa ya tatizo hili ni Network Failure. je kwa upande wetu sisi watanzania tatizo hili lipo? watumiaji wa blackberry tunapenda kujua kama na nyinyi pia  mme experience tatizo hili 
Tell us!Sunday, May 22, 2011

TOFAUTI KATI YA LAPTOP NA NETBOOK

Analyst wetu anatuelezea tofauti kati ya laptop na netbook, hii imekuwa ikichanganya baadhi ya watu haswa katika maamuzi ya ununuaji wa computer.

JE NI VITU GANI VYA KUANGALIA ILI UWEZE KUTOFAUTISHA LAPTOP NA NETBOOK?

Kwanza kabisa Netbook huwa ni ndogo mara nyingi zinakuwa na ukubwa wa 7" - 12" wakati Laptop zinakuwa na ukubwa wa 14"  na kuendelea.

Kitu cha pili cha kuangalia ambacho kinatakuwezesha kutofautisha Netbook na Laptop ni Processor, Laptop inakuwa na uwezo wa ku process information nyingi zaidi kwa hiyo inamuwezesha mtumiaji kuangalia Program nyingi zaidi kwa mfano Movies na Games. wakati kwenye Netbook inakuwa ni vigumu.

Kitu cha tatu cha kuangalia ni Keyboard, Keyboard ya Netbook ni ndogo kuliko ya Laptop hata kama ukijaribu kutype kwenye netbook kama ni mtu mwenye vidole vikubwa inakuwa vigumu kidogo wakati kwenye Laptop unakuwa comfortable zaidi katika uchapaji wa kazi au wakati unatumia Laptop kwa shughuli kama za ku browse internet.

kitu cha nne cha kuangalia ni Hard Drive; Laptop inatumia Hard Disk Drive wakati Netbook inatumia SSD. inasemekana kuwa SSD ziko fasta sana kwenye ku access au kuleta data.

Kitu cha tano ni Disk Drive; Laptop zinakuja na disk drive ambazo zinawezesha kusoma na kutengeneza CD na DVD, wakati Netbook hazina CD-ROM/DVD disk drive, kwa hiyo kama mtu anataka ku play movie hii haitawezekana kwa kuwa netbook haina feature hiyo. mtumiaji wa Netbook kama anataka kuangalia movie inabidi atumie external disk drive kupitia port ya USB.


 

Sunday, March 13, 2011

Tanzania as a place for low quality product including High Tech Products

Find the list of links above on each of those list you will be able to understand the product you are aiming to get.